Wimbo wa Mapambano (Movements Anthem)
Kupigwa na kupokonywa maisha
Hakutatuzuia sisi wananchi
Kupigania Uhuru wetu
Na haki ya jasho letu
(Jasho Letu)
Na haki ya jasho letu
Tumekataa kupiga magoti
Mbele ya hawa wauaji
Bila shaka sisi pia ni watu
Hali ya utumwa tumeikataa
(Kata Kata)
Hali ya utumwa tumeikataa
Tutanyakuwa mashamba yetu
Tupiganie Uhuru wetu
Tuikomboe elimu yetu
Utamaduni na viwanda vyetu
(Tukomboe)
Utamaduni na viwanda vyetu
Sisi hatutaki kudhulumiwa
Hatutaki tena mauaji
Hili kupe tuliangushe
Haki na Uhuru tuchanue
(Tuchanue)
Haki na Uhuru tuchanue
Uhuru Wetu, Afreeka Afreeka, Uhuru we-tu Afreeka tupiganie
Mashamba Yetu, Afreeka Afreeka, Masamba ye-tu Afreeka tupiganie
Maisha Yetu, Afreeka Afreeka, Maisha ye-tu Afreeka tupiganie